5.7 C
New York

Mwandishi aliyeingia kazini akiwa amelewa aomba radhi

Published:

MILAN, Italia

MWANDISHI wa habari raia wa Italia, Danika Mason, ameomba radhi baada ya video iliyosambaa mitandaoni kumuonesha akiwa amelewa pombe.

Mason ni miongoni mwa waandishi wa kituo cha runinga cha Channel Nine walioko Italia kuripoti michuano ya Olimpiki.

Video iliyomponza, ambayo hata Waziri Mkuu wa Australia ameilaani, inamuonesha Mason akipata wakati mgumu kutamka baadhi ya maneno kwa kuzidiwa na pombe.

Akiomba radhi kupitia mitandao ya kijamii, amekiri kufanya kosa na kusema anapaswa kuwajibishwa kwa kile kilichotokea.

“Napaswa kuwajibika, sio utendaji niliojiwekekea. Imenidhalilisha,” amesema Mason.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img