6.4 C
New York

Raia Urusi walia ugumu wa maisha

Published:

MOSCOW, Urusi

“MAISHA yamekuwa ghali mno.” Ni kauli ya Alexander, mkazi wa mjini Moscow, ambaye ni mtaalamu wa moja ya kampuni kubwa za matangazo nchini Urusi.

Kwa kipindi cha mwezi mmoja, bajeti ya chakula imepanda kwa asilimia 22, kutoka Dola za Marekani 450 hadi Dola 555.

Wachambuzi wa uchumi wanasema kupanda kwa gharama za maisha kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na vita kati ya Urusi na Ukraine.

Ikielezwa, kupanda huko kwa bei ya bidhaa za vyakula kunatokana na fedha nyingi kuelekezwa katika kuishambulia Ukraine na sekta ya ulinzi.

Mbali ya hilo, pia wachambuzi wanataja vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa Urusi na mataifa ya Magharibi na kudorora kwa kasi ya wawekezaji kutoka nje.

Gharama hizo zinagusa bidhaa muhimu, yakiwamo mayai, nyama ya kuku na ng’ombe, maziwa, sabuni, chumvi, dawa ya mswaki, ndizi na hata mboga za majani.

Kwa maduka makubwa (supermarket), gharama za bidhaa zinatajwa kupanda kwa asilimia 2.6 ndani ya mwezi mmoja.

Kwa upande mwingine, mfumuko wa bei za bidhaa unaripotiwa zaidi katika maeneo ya mijini, kwa maana ya Moscow na St Petersburg.

Huku wasio na ajira wakiwa hoi, hali ni mbaya hata kwa watumishi, ambao wanalalamika kuwa mishahara inakinzana na gharama halisi za maisha.

Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Alexander anasema siku hizi anashindwa kutoka na mkewe kwenda kupata chakula migahawani.

“Hata bajeti ya kupika nyumbani imeongezeka kutoka Dola 12.29 hadi zaidi ya Dola 25.85,” anasisitiza Alexander.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img