6.4 C
New York

Mgomo wa wafanyakazi wachelewesha safari za ndege

Published:

NAIROBI, Kenya

MGOMO wa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta umesababisha kuchelewa kwa baadhi ya safari.

Kama itakumbukwa, wiki iliyopita Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya ilijaribu kuiomba Mahakama itoe amri ya kuzuia mgomo huo.

Mbali ya madai mengine, Umoja wa wafanyakazi wa viwanja wa ndege nchini Kenya umeandaa maandamano hayo kushinikiza nyongeza ya mishahara.

Kwa upande wake, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya imeahidi kumaliza changamoto hiyo ya mgomo kwa kukaa mezani na wahusika.

Kutokana na ukubwa na wingi wa ndege unaozihudumia, Uwanja wa Jomo Kenyatta unatajwa kuwa ni kitovu cha usafiri wa anga barani Afrika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img