8.2 C
New York

Mastaa wa soka wanaotokea familia tajiri Ulaya

Published:

LONDON, Uingereza

MCHEZO wa soka una historia kubwa ya kuwainua na kuwapa utajiri wachezaji wanaotoka katika familia za kimasikini.

Miongoni mwao ni mkongwe wa soka la Argentina, Diego Maradona. Pia, ipo historia ya maisha magumu aliyowahi kupitia mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Victor Moses.

Orodha ya wachezaji wa aina hiyo ni ndefu lakini kwa upande mwingine kuna ambao waliingia katika mchezo wa kandanda wakitokea katika familia zenye maisha bora.

Frank Lampard

Kiungo huyo wa kimataifa wa England ndiye mfungaji bora wa muda wote katika historia ya klabu ya Chelsea. Alitwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya England akiwa na Blues.

Hata kabla ya kuibuliwa na West Ham United na kisha kutua Chelsea mwaka 2011, baba yake aitwaye Frank alishakuwa kocha Ligi Kuu ya England. Ni kama ilivyokuwa kwa mjomba wake, Harry Redknapp.

Kama si soka, Lampard angekuwa mchumi kwani wazazi wake walimsomesha katika moja ya shule za gharama kubwa nchini Uingereza.

Gianluca vialli

Ni mkongwe mwingine wa Chelsea, ambaye alicheza katika klabu za Cremonese, Sampdoria na Juventus, kabla ya kutua London mwaka 1996.

Nje ya soka, Muitalia huyo alikulia katika nyumba ya kifahari ya baba yake huko Kaskaini mwa nchi hiyo. Ni nyumba iliyokuwa na vyumba vya kulala 60 iliyofahamika kwa jina la Castello di Belgioioso.

Gerard Pique

Beki huyo wa zamani wa Barcelona anatokea familia ambayo baba ni mwanasheria na mama ni mkurugenzi wa hospitali kubwa mjini Barcelona.

Ifahamike kuwa babu yake ni Amador Bernabeu, ambaye aliwahi kushika nafasi ya makamu wa rais wa Barcelona. Kwa Pique, soka lilikuwa ni starehe tu, na si njia ya kujikwamua kimaisha.

Hugo Lloris

Kipa wa zamani wa Tottenham, ambaye kwa sasa anakipiga Ligi Kuu ya Marekani. Aliiongoza timu ya taifa ya Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2018.
Lloris anatokea katika familia ambayo baba ni mtaalamu wa masuala ya uchumi na mama ni mwanasheria. Akiwa mdogo, alipenda zaidi mchezo wa tenesi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img