10.4 C
New York

Leicester City wamkimbia staa wa filamu za ngono

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Leicester City imevunja mkataba wake na jezi na BC Game baada ya kampuni hiyo kumtangaza staa wa filamu za ngono kuwa balozi wake.

BC Game, kampuni ya ‘kubeti’ ambayo ilianza kufanya kazi na Leicester City mwanzoni mwa msimu wa 2024-25, ilimtangaza mrembo Eva Elfie kuwa balozi mapema mwezi huu.

Katika taarifa yake wakati inamtangaza Eva, kampuni hiyo ilieleza kuwa kamari na ngono ni maeneo yenye nafasi kubwa, hasa kwa kundi la vijana, hivyo ni vizuri kufanya kazi pamoja.

“Mahusiano kama haya yanaleta pamoja dunia mbili kubwa tofauti na kuziunganisha na Leicester City. Hapa ndiko tuliko sasa,” ilieleza taarifa ya BC Game.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Leicester, mashabiki waliokwishanunua jezi ndani ya siku 28 zilizopita watabadilishiwa.

Related articles

Recent articles