NAIROBI, Kenya
KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, Benni McCarthy, amesema haumizwi kichwa na wanaoponda kiwango kibovu kinachooneshwa na timu hiyo.
Mashabiki wa timu hiyo wamekerwa na matokeo ya kukosa ushindi katika mechi mbili walizocheza hivi karibuni dhidi ya Bafana Bafana.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Afrika Kusini, timu hizo zilitoka suluhu [0-0], kabla ya Harambee Stars kufungwa mabao 2-1 ikiwa nyumbani juzi.
Licha ya kusema hana presha, McCarthy alishuhudia akizomewa na mashabiki baada ya dakika 90 za mechi hiyo ya pili iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nyayo.
Akizungumza na waandishi wa habari, McCarthy, straika wa zamani wa Manchester United na Bafana Bafana, alisema kelele hizo hazijaweza kumzuia kupanga usingizi mzuri awapo nyumbani.
“Ninaporudi nyumbani, naweka mto wangu na kulala vizuri kama mtoto,” amesema McCarthy. “Maisha yangu yamekamilika. Siwezi kuhofia presha za aina hii.”


