10.9 C
New York

Merino, Zubimendi kumpisha ‘mido’ mpya Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

ARSENAL watachagua nani wa kumuuza kati ya Mikel Merino na Martin Zubimendi ili kumpa nafasi kiungo wa Bournemouth, Alex Scott, kwa mujibu wa Gazeti la Sun.

Arsenal wanaipambania saini ya Scott, usajili ambao utailazimisha klabu hiyo kumuuza mmoja kati ya Merino na Zubimendi.

Kwa sasa, vita ni kali ya Arsenal, Chelsea na Liverpool, ambazo kila moja inaitaka huduma ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 23.

Ripoti zinaeleza kuwa klabu zote tatu zimeshafanya mawasiliano na uongozi wa Bournemouth kuzungumzia dili hilo.

Kwa upande wa Arsenal, kocha wake, Mikel Arteta, amejadili na Mkurugenzi wa Michezo, Andrea Berta, juu ya umuhimu wa Scott kwenye mipango yao ya msimu ujao.

Related articles

Recent articles