AMSTERDAM, Uholanzi
KAMPUNI binafsi ya Autoriteit Persoonsgegevens (AP) ya nchini Uholanzi imelaani matumizi ya miwani ya kisasa iliyotengenezwa kwa teknolojia ya akili-unde [AI].
Katika uchunguzi wake kwa aina sita tofauti, bila kutaja kampuni zilizotengeneza, AP imebaini kuwa miwani hiyo inampotosha kwa kiwango kikubwa mtu aliyeivaa.
Miongoni mwa kasoro zilizobainishwa na AP, miwani hiyo inashawishi mtumiaji kujingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na watoto wadogo na inapotosha usomaji wa maelekezo ya dawa.
Pia, utafiti wa AP umebaini kuwa si kweli kwamba ina uwezo wa kuita gari la wagonjwa [ambulance] kama inavyoahidiwa katika matangazo yake.
Hivyo, ushauri wa AP umewataka wananchi wa Uholanzi kuacha mara moja kununua miwani hiyo, pia ikiiomba Serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku uuzwaji wake.
Licha ya kutoweka hadharani majina ya kampuni, AP imeeleza kuwa miwani isiyostahili kuuzwa ni ya bei chini ya euro 100 hadi euro 500.
Utafiti wa Taasisi hiyo unakuja huku tayari kukiwa na mjadala mkubwa wa kupinga miwani za AI, ambazo nyingi zimetajwa kuwa na kamera za siri zinazomruhusu mtumiaji kurekodi pasi na kupewa ruhusa.


