18.1 C
New York

UN: Wasichana milioni 4.5 hatarini kukeketwa mwaka 2026

Published:

NEW YORK, Marekani

RIPOTI mpya ya Umoja wa Mataifa (UN) inaonesha kuwa wasichana takribani milioni 4.5 duniani kote wako kwenye hatari ya kufanyiwa ukeketaji kwa mwaka huu wa 2026.

Wakati huo huo, ripoti hiyo ya UN kupitia Shirika lake la Kuhudumia Watoto (UNICEF) imeeleza kuwa wengi kati ya wasichana hao ni wenye umri chini ya miaka mitano.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanawake na wasichana milioni 230 ni wahanga wa matukio hayo.

Vitendo vya ukeketaji, kwa mujibu wa UNICEF, yamekuwa kwa kiwango kikubwa katika maeneo ya Afrika Mashariki na Asia, yakihusishwa na mila potofu.

“Watoto wenye umri chini ya miaka mitano wamekuwa wahanga wakubwa na wanaachiwa madhara yanayowatesa kwa muda mrefu,” inaeleza taarifa ya UNICEF.

Aidha, Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) limelaani vitendo hivyo likisema: “Ukeketaji ni ukiukwaji wa haki za binadamu na hauvumiliki kwa namna yoyote ile.”

“Vitendo hivyo vinawaacha wasichana na wanawake kwenye maumivu makubwa ya kimwili na kisaikolojia …”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img