10.7 C
New York

Rosenior atangazwa kocha mpya Chelsea

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Chelsea imemtangaza, Liam Rosenior kuwa kocha mpya atakayechukua mikoba ya Enzo Maresca.

Rosenior amejiunga na Chelsea akitokea Strasbourg, ambayo pia inamilikiwa na mabosi wa klabu hiyo ya London.

Kocha huyo raia wa Uingereza ametua Stamford Bridge na kusaini mkataba wa miaka sita na nusu. Utakwisha mwaka 2023.

“Nimefurahi kuona nimeheshimiwa kwa kuajiriwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Chelsea,” amesema Rosenior mwenye umri wa miaka 41.

Wakati huo huo, Rosenior amefichua kuwa ataongozana na wasaidizi wake aliokuwa nao Strasbourg, ambao ni Kalifa Cisse, Justin Walker na Ben Warner.

Kabla ya kutangazwa, aliwahi kuizungumzia uwezekano wa kuinoa Blues katika siku za usoni, akisema asingeweza kukataa ofa ya kufanya kazi na vigogo hao wa Ligi Kuu ya England.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img