MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI Kylian Mbappe amebaki nyumbani wakati kikosi cha Real Madrid kiliposafiri kwenda Saudi Arabia kwa mchezo wao wa Spanish Super Cup.
Madrid watakuwa nchini humo kwa ajili ya ‘derby’ ya Alhamisi hii dhidi ya wenzao wa La Liga, Atletico Madrid.
Kocha wa Madrid, Xabi Alonso, amemwacha Mbappe kwa kuwa bado anauguza majeraha ya mguu.
Pia, beki wa pembeni wa timu hiyo, Trent Alexander-Arnold, hajajumuhishwa kikosini, sababu ikiwa ni hiyo ya majeraha.
Hata hivyo, habari njema kwa Madrid ni kurejea kwa mlinzi wake wa pembeni, Dani Carvajal, ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili.


