10.7 C
New York

Ferdinand ataja kocha mpya United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

NAHODHA wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, anaamini Darren Fletcher anatosha kuibeba timu hiyo baada ya Ruben Amorim kutimuliwa.

Amorim amefutwa kazi baada ya miezi 14 tu ya kuliongoza benchi la ufundi la ‘Mashetani Wekundu’ wa Old Trafford.

Taarifa ya Mreno huyo kufungashiwa virago ilikuja muda mfupi tu baada ya Manchester United kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Leeds United wikiendi iliyopita.

Kwa sasa, Fletcher anayeinoa U-18 ya timu hiyo ndiye aliyekabidhiwa mikoba wakati mabosi wakiendelea kusaka kocha mpya.

Hata hivyo, Ferdinand aliyewahi kucheza na Fletcher wakiwa Manchester United misimu mingi iliyopita, anaamini mkongwe mwenzake huyo anatosha kupewa mkataba wa kudumu.

Wakati huo huo, amesema si mbaya pia endapo uongozi wa klabu hiyo utamtafuta Roberto De Zerbi, Thomas Tuchel au Xavi.

Aidha, kuondoshwa kwa Amorim ni mwendelezo wa nyakati ngumu wanazopitia makocha walioajiriwa tangu Alex Ferguson alipoondoka Old Trafford.

Iko wazi kuwa Manchester United imetumia zaidi ya Pauni milioni 50 kuwalipa fidia makocha iliovunja nao mikataba tangu Ferguson alipostaafu mwaka 2013.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img