15 C
New York

Manchester United yamfuta kazi Amorim, Fletcher akabidhiwa mikoba

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KLABU ya Manchester United imethibitisha kuachana na kocha wake mkuu, Ruben Amorim, katika uamuzi uliokuja kwa masikitiko lakini ukilenga maslahi ya baadaye ya klabu hiyo kongwe ya England.

Amorim aliteuliwa kuinoa Manchester United Novemba 2024 na katika kipindi chake aliiongoza timu hiyo kufika Fainali ya Ligi ya Europa ya UEFA iliyochezwa mjini Bilbao mwezi Mei, mafanikio yaliyompa heshima kubwa miongoni mwa mashabiki.

Hata hivyo, huku United ikiwa nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (Premier League), uongozi wa klabu umeamua kuwa huu ni wakati muafaka wa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi ili kuipa timu nafasi bora zaidi ya kumaliza ligi katika nafasi ya juu kadri inavyowezekana.

Kupitia taarifa yake, klabu imemshukuru Amorim kwa mchango wake mkubwa katika kipindi kifupi alichohudumu Old Trafford, na kumtakia kila la heri katika hatua inayofuata ya maisha na taaluma yake ya ukocha.

Kwa sasa, Darren Fletcher amekabidhiwa jukumu la kuinoa timu kwa muda na ataiongoza Manchester United katika mchezo ujao dhidi ya Burnley utakaochezwa Jumatano.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img