MADRID, Hispania
BADO mabosi wa Real Madrid wanaumiza vichwa juu ya mpango wao wa kuinasa saini ya kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Hispania, Rodrigo Hernández.
Kwa muda mrefu sasa, Rodri ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or mwaka jana, amekuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaoitoa udenda Madrid.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, amebakiza miezi 18 katika mkataba wake na Manchester City lakini klabu hiyo haina mpango wa kumuuza.
Hata hivyo, mazungumzo ya mkataba mpya yanapaswa kukamilika miezi sita au nane ijayo ili kuepuka hasara ya kumpoteza akiwa mchezaji huru mwaka 2027.
Madrid, kwa upande wao, wamekuwa kwenye mawindo ya kutafuta mchezaji sahihi wa kuziba pengo la Toni Kross aliyetangaza kustaafu mwaka jana.
Rodri amekuwa mchezaji muhimu katika eneo la kiungo wa ulinzi tangu Manchester City ilipomsajili mwaka 2019 akitokea La Liga alikokuwa akiitumikia Atletico Madrid.


