15 C
New York

Chiesa aibukia AS Roma

Published:

ROMA, Italia

KLABU ya AS Roma imemuweka kwenye rada zake kiungo wa pembeni wa Liverpool raia wa Italia, Federico Chiesa.

Wakati huo huo, nyota huyo anahusishwa na Juventus, ingawa Roma imetajwa kuwa mstari wa mbele zaidi katika mbio za kumsajili.

Roma ilimtaka Chiesa tangu wakati wa usajili wa kiangazi, mwaka jana, lakini Liverpool iligoma kumwachia nyota huyo mwenye umri wa miaka 28.

Usajili wa Chiesa umelenga kuziba pengo la Leon Bailey, ambaye hajaweza kuwa na kiwango kizuri tangu aliposajiliwa na Roma akitokea Aston Villa.

Ni kwa maana hiyo, endapo Chiesa atasajiliwa Januari hii, ni wazi Bailey raia wa Jamaica atafingasha virago vyake klabuni hapo.

Licha ya kiwango chake bora katika mechi alizopata nafasi, Chiesa anapata wakati mgumu kujihakikishia namba ya kucheza kikosi cha kwanza pale Anfield.

Alijiunga na Liverpool mwaka jana akitokea Juventus kwa Pauni 12 na msimu huu ameingia kikosi cha kwanza mara moja pekee katika mechi za Ligi Kuu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img