LONDON, Uingereza
MABOSI wa Chelsea wameripotiwa kuanza harakati za kumchukua kocha wa Newcastle United, Eddie Howe.
Wakati huo huo, taarifa zinaeleza kuwa wanaitaka saini ya kiungo wa timu hiyo, Sandro Tonali.
Kwa sasa, Blues hawana kocha mkuu baada ya kumfungashia virago Enzo Maresca akiwa amehudumu kwenye benchi kwa miezi 18 pekee.
Howe anaungana na orodha ndefu ya makocha wanaotajwa Stamford Bridge, akiwamo Zinedine Zidane, ambaye amekuwa nje ya kazi kwa muda mrefu.
Aidha, mtandao wa Football Insider umedai kuwa usajili wa Tonali mwenye umri wa miaka 25 utafanyika mwishoni mwa msimu huu ili kuwaongezea nguvu Cole Palmer, Moises Caicedo na Enzo Fernandez.
Hata hivyo, Blues watalazimika kutumia mkwanja mrefu kumpata kwani mkataba wake na Newcastle utakwisha mwaka 2029.


