15 C
New York

Baleba aingia rada za Liverpool

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

LIVERPOOL imeungana na Manchester United na Tottenham katika mbio za kumsajili kiungo wa Brighton na timu ya taifa ya Cameroon, Carlos Baleba.

Brighton haijakataa uwezekano wa kumwachia Baleba lakini imesisitiza kuwa mchezaji huyo atauzwa endapo itatokea klabu ya kuipa kitita cha euro milioni 100.

Taarifa zingine zinaeleza kuwa Brighton hawako tayari kumfungulia mlango wa kutokea kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo la Januari, na badala yake watasubiri hadi mwishoni mwa msimu huu.

Vigogo wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), Bayern Munich, nao ni miongoni mwa klabu zinazotajwa kuitolea macho huduma ya nyota huyo.

Kwa upande wa Manchester United, kocha Ruben Amorim anaamini Baleba atakuwa na nafasi kubwa ya kucheza mbele ya Casemiro na Manuel Ugarte.

Kocha wa Liverpool, Arne Slot, anamtaka staa huyo ili kumpa ushindani wa namba kiungo wake raia wa Uholanzi, Ryan Gravenberch.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img