15 C
New York

Man City v Chelsea … Shoo ya kibabe Etihad

Published:

MANCHESTER Uingereza

MANCHESTER City itakuwa nyumbani katika Uwanja wa Etihad kukaribisha Chelsea, mchezo wa Ligi Kuu ya England utakaochezwa wikiendi hii (Januari 5, 2026).

Kwa upande wao, Manchester City wako nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi, wakizidiwa pointi nne na Arsenal waliokaa kileleni. Blues wao wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo, wakiwa wameachwa pointi tatu na Liverpool iliyo juu yao.

Aidha, Manchester City ya Pep Guardiola itarejea dimbani ikiwa imetoka kulazimishwa suluhu (0-0) na Sunderland.

Chelsea, kwa upande wao, watakwenda Etihad wakiwa na maumivu kama hayo kwani walilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Bournemouth katika mchezo uliopita.

Pigo kubwa zaidi kwao ni kwamba wataivaa Manchester City wakiwa bila kocha mkuu baada ya kumfuta kazi Enzo Maresca.

Kufukuzwa kwa Muitalia huyo kumempa nafasi kocha wa Unde-21, Calum McFarlane, ambaye ndiye atakayeliongoza benchi la ufundi la Blues katika mchezo dhidi ya Manchester City.

Kama hiyo haitoshi, wakali hao wa Stamford Bridge wameshinda mechi moja pekee kati ya saba za Ligi Kuu walizocheza hivi karibuni.

Mbaya zaidi, hata rekodi hazipo upande wao. Chelsea haijaifunga Manchester City katika michuano yoyote tangu mwaka 2021.

Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa Januari, mwaka jana, ambapo Blues walifungwa mabao 3-1 katika Uwanja wa Etihad.

Katika mchezo huo, Blues walitangulia kwa bao la Noni Madueke, kabla ya Erling Haaland na Phil Foden kuifungia Manchester City na kuipeleka nafasi ya nne kwenye msimamo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img