AMSTERDAM, Uholanzi
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana, Andre Ayew, amejiunga na NAC Breda inayoshiriki Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie).
Ayew mwenye umri wa miaka 36, amesaini mkataba utakaokwisha mwishoni mwa msimu huu na ni baada ya miezi mitano akiwa hana klabu.
Staa huyo anaikuta timu hiyo ikiwa kwenye hali mbaya kwani imekusanya pointi 13 pekee katika mechi 17 za msimu huu wa Ligi Kuu ya Uholanzi.
“Mimi ni mtu ninayependa changamoto … Nataka nifanye kila linalowezekana kuisaidia klabu na wachezaji wenzangu,” amesema.
Kwa Ayew, NAC Breda inakuwa klabu yake ya 10 katika safari yake ya soka la kulipwa tangu alipoibuliwa na Marseille ya Ufaransa.
Tangu alipoondoka Marseille, ameitumikia Lorient, Arles-Avignon, Le Havre, Swansea City, West Ham United, Nottingham Forest, Fenerbahce na Al Sand.


