22 C
New York

Yatakayojiri ulimwengu wa michezo 2026

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

HATIMAYE miezi 12 ya mwaka 2025 imetamatika. Mwaka huu, 2026, una matukio mengi ya kusubiriwa kwa hamu na wapenzi wa michezo duniani kote.

GAZETINI kwa msaada wa mashirika ya habari ya kimataifa, inakueletea matukio hayo. Endelea kusoma.
Australian Open (Jan 12-Februari Mosi).

Jannik Sinner atasaka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili baada ya Novak Djokovic kutwaa mara tatu mfululizo taji la michuano hiyo ya tenesi.

Kwa upande wa wanawake, Madison Keys atapambana kutetea taji alilobeba mwaka jana kwa kumfunga Aryna Sabalenka.

Formula One (Machi 6-Desemba 6)

Mashindano ya dunia ya mbio za magari. Michuano hiyo itakayoanzia Australia na kuishia Abu Dhabi (Falme za Kiarabu), itahusisha mbio 24.

Je, mtaalamu wa mbio za magari, Lando Norris, ataibuka bingwa wa dunia kama alivyofanya mwaka 2025?
Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya (Mei 22)

Ni kwa upande wa soka la wanawake na itachezwa katika Uwanja wa Ullevaal mjini Oslo, Norway. Arsenal ni mabingwa watetezi baada ya kuifunga Barcelona msimu uliopita.

Kwa sasa, baadhi ya timu kwenye michuano hiyo zimeshatinga hatua ya robo fainali. Arsenal watatakiwa kuifunga OH Leuven ili kufika hatua hiyo.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa wanaume itachezwa Mei 30. Arsenal wako kileleni mwa Kundi wakiwa wameshinda mechi zote sita.

Haa hivyo, bado kuna ushindani mkali kutoka kwa Bayern Munich, PSG, Real Madrid, Barcelona, Manchester City na Liverpool.

Kombe la Dunia (Juni 11-Julai 19)

Kwa mara ya kwanza, michuano hiyo itakuwa na wenyeji watatu (Marekani, Canada na Mexico). Pia, ni historia kuona itashirikisha timu 48.

Scotland itashiriki kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28 kupita. England nayo itajaribu kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1966.

Wimbledon (Juni 29-Julai 12)

Michuano mikongwe katika ulimwengu wa tenesi. Safari hii, ni vita ya mastaa Jack Draper, Cameron Norrie, Emma Raducanu na Katie Boulter. Wakati huo huo, wanatazamiwa kupata ushindani mkali kutoka kwa Carlos Alcaraz, Sinner, Sabalenka na Iga Swiatek.

Michezo ya Jumuhiya ya Madola (Julai 23-Agosti 2)

Itafanyika kwa mara ya kwanza mjini Glasgow, Scotland, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014. Ni michuano inayoshirikisha mataifa 74, michezo 10 na wanamichezo 3,000.
Tofauti na ilivyokuwa mwaka 2014, safari hii michuano hiyo itakosa michezo saba, ukiwamo wa kunyanyua vitu vizito kwa watu wenye ulemavu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img