18 C
New York

Ake wa Man City agombewa EPL

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU kadhaa za Ligi Kuu ya England (EPL), ikiwamo Bournemouth, zimeonesha nia ya kumsajili beki wa kati aliyepoteza namba katika kikosi cha Manchester City, Nathan Ake. Ake hajui hatima yake klabuni hapo kwani amecheza mara moja pekee katika ‘first eleven’ ya Man City msimu huu wa EPL.

Kwa sasa, akili yake iko kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia lakini anafahamu wazi kuwa hawezi kuitwa katika kikosi cha Uholanzi ikiwa anasota benchi pale Etihad.

Mlinzi wa kati huyo alicheza mechi zaidi ya 100 za EPL akiwa na Bournemouth, kabla ya Man City kumsajili kwa ada ya Pauni milioni 41 mwaka 2020.

Bournemouth inahitaji beki wa kati mpya wa kuchukua nafasi ya Marcos Senesi anayetaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu. Crystal Palace nayo inatajwa kuimezea mate huduma ya Ake ikiamini atawafaa kuziba pengo la Marc Guehi anayeweza kuondoka Januari, mwakani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img