9.8 C
New York

Stars yaanza vibaya AFCON, Bacca amficha Osimhen

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeanza vibaya msimu huu wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Nigeria ‘Super Eagles’.

Ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Kundi C, kabla ya Uganda kuivaa Tunisia, Eagles walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Semi Ajayi aliyefunga dakika ya 36 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Alex Iwobi.

Staa wa Eagles, Victor Osimhen, alikaribia kuindikia timu yake bao la pili, kabla ya mwamuzi kubaini kuwa straika hiyo alishaotea kabla ya kukwamisha mpira kimiani.

Katika dakika ya 52, Stars walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Charles M’Mombwa aliyeunganisha krosi ya Novatus Dismas. Sekunde chache baada ya bao hilo, nyota wa Eagles, Ademola Lookman, alifunga bao la ushindi kwa timu yake kwa shuti kali nje kidogo ya boksi.

Mbali ya kiwango bora cha Stars, kivutio kingine cha mchezo huo ni namna beki wake wa kati, Ibrahim Hamad ‘Baca’ alivyokuwa akimpa wakati mgumu Osimhen. Katika matukio mengi ya mshambuliaji huyo wa Galatasaray kuwa karibu na lango la Stars, Bacca alifanikiwa kufika na kumnyima uhuru wa kupiga.

Haikushangaza kuona Osimhen akiitwa benchi katika dakika ya 86 ya mchezo, ilionesha kuwa mambo yalikuwa magumu kwa upande wake.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img