18 C
New York

Mastaa Man City kupimwa uzito

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, ameweka wazi kuwa wachezaji wake wote watapimwa uzito, kabla ya mchezo wao dhidi ya Nottingham Forest. Timu hizo zitashuka dimbani Desemba 27, mwaka huu, siku mbili baada ya shamrashamra za Sikukuu ya Krismas.

Kwa mujibu wa Guardiola, utaratibu huo wa kuwapima uzito wachezaji ulifanyika pia kabla ya mechi yao iliyopita dhidi ya West Ham United. Walishinda mabao 3-0.

“Endapo mchezaji atakuwa ameongezeka uzito, basi atabaki jijiji Manchester, hatosafiri na timu kuifuata Nottingham Forest,” amesema.

Guardiola anafahamika kwa msimamo wake juu ya nidhamu ya utimamu wa mwili kwa wachezaji, kama alivyofanya mwaka 2016.

Wakati huo, Mhispania huyo aliwaondosha kikosini baadhi ya wachezaji wake muhimu baada ya kubaini kuwa wameongezeka uzito.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img