18 C
New York

Krismas na maajabu yake EPL

Published:

LONDON, Uingereza

KWA mashabiki wa Ligi Kuu ya England (EPL), Sikukuu ya Krismas imekuwa na historia ya pekee kwao. Kivipi?
Timu inayokuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi kufikia siku ya Krismas, kwa maana ya Desemba 25, imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Ndiyo, katika misimu 33 ya hivi karibuni, timu zote zilizokuwa kileleni kufikia Krismas, ziliishia kuwa mabingwa wa Ligi Kuu hiyo inayofuatiliwa zaidi duniani.

Safari hii, ni Washika Bunduki wa London, Arsenal, ndiyo wako kileleni na Krismas itawakuta wakiwa hapo. Je, ni mabingwa watarajiwa?

Kwa upande mwingine, timu iliyoshika nafasi ya pili kwenye msimamo kufikia Krismas, ni nadra kufanikiwa kutwaa ubingwa.

Ndiyo, kwa misimu 17 ya hivi karibuni, ni mara mbili pekee zilizotwaa ubingwa baada ya kushika nafasi ya pili siku ya Krismas. Ni Manchester City pekee walioweza kufanya hivyo.

Wakati huo huo, Sikukuu ya Krismas imekuwa ikitoa picha pia juu ya timu zinazoweza kushuka daraja EPL.
Kwa misimu 33 iliyopita, ni timu nne pekee ambazo zilipona baada ya Krismas kuzikuta kwenye nafasi za kushuka daraja. Wolves ni moja ya timu hizo iliponusurika msimu wa 2022-23.

Ukitazama msimamo wa sasa, Wolves, Burnley na West Ham ndizo zilizo kwenye nafasi mbaya na Krismas itazikuta hapo. Je, ni kwamba nazo zitaiaga EPL?

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img