18 C
New York

Barcelona yatua Misri, yamtaka kinda Al Ahly

Published:

CATALUNYA, Hispania

BARCELONA imeanza harakati za kumsajili kinda wa Al Ahly ya Ligi Kuu nchini Misri, Hamza Abdelkarim.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 17, amecheza mechi nne pekee akiwa na timu ya wakubwa ya Al Ahly.

Hata hivyo, Abdelkarim amekuwa kwenye kiwango bora akiwa na timu za vijana, pia akifunga mabao 12 katika mechi 17 za U-17 ya Misri.

Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Barcelona wanavutiwa na kiwango chake na wametenga euro milioni nne kuinasa saini yake.

Kwa upande mwingine, Al Ahly na Barcelona hawajafikia makubaliano juu ya mchezaji huyo kwenda Hispania ifikapo Januari, mwakani.

Gazeti la SPORT la Hispania limedai kuwa Al Ahly hawakatai kumwachia, bali wameiambia Barcelona isubiri hadi Juni, mwakani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img