9.8 C
New York

Simulizi za AFCON (6): Mastaa na vitendo vya ushirikina

Published:

LAGOS, Nigeria

MADAI ya vitendo vya kishirikina si jambo geni katika historia ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON). Hii ikoje? Endelea kusoma.

Wakati wa fainali za AFCON za mwaka 2000, mmoja ya viongozi wa timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ aliondoka kwenye benchi na kuingia uwanjani.

Kiongozi huyo alinaswa na kamera za uwanjani akienda kutoa kitu (inasemekana ni hirizi) nyuma ya lango la wapinzani wao, Senegal.

Itakumbukwa pia, wakati wa fainali za AFCON za mwaka 2008, mashabiki wa timu ya taifa ya Ghana walionekana wakiwa na vyungu vilivyokuwa na majivu, wakidai ni kwa ajili ya kuondosha uchawi wa wapinzani wao.

Kama hiyo haitoshi kuhusu Ghana, mshambuliaji wake, Andre Ayew, alifanya tukio la kishiriki wakati wa fainali za mwaka 2015. Alionekana alikwaga ‘unga’ ndani ya uwanja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img