NDOLA, Zambia
MASHABIKI wa soka nchini Zambia wataendelea kuitunza kwenye kumbukumbu zao Aprili 27, 1993. Ilikuwaje siku hiyo? Endelea kusoma.
Siku hiyo, wachezaji wa timu ya taifa ‘Chipolopolo’ walikuwa safarini kwenda Senegal kwa ajili ya mchezo wao wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Isivyo bahati, ndege waliyokuwamo ilipata ajali ikiwa umbali mdogo tu wa meta 500 kuufikia Mji Mkuu wa Gabon, Libreville.
Ni ajali iliyokatisha uhai wa wachezaji wote 25, pia ikisababisha vifo vya wahudumu watano wa ndani ya ndege hiyo.
Ilikuwa ni simanzi kubwa kwa Zambia kwani tayari timu hiyo ilitoka kuifunga Italia katika michuano ya Olimpiki, hivyo matumaini ya kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza yalikuwa makubwa.
Hata hivo, ndani ya mwaka mmoja, Chipolopolo ni kama ‘ilizaliwa upya’ kwani ilifika fainali kwenye michuano ya AFCON ya mwaka 1994. Ilifungwa mabao 2-1 na Nigeria katika mchezo wa fainali.


