15 C
New York

Mabosi wa Messi wamsajili beki Tottenham

Published:

MIAMI, Marekani

INTER Miami ya Marekani imemsajili mlinzi wa kushoto wa zamani wa Tottenham na Real Madrid, Sergio Reguilon, akiwa mchezaji huru.

Reguilon mwenye umri wa miaka 28, amekuwa hana klabu tangu alipoachwa na Tottenham mwishoni mwa msimu uliopita.

Kwa upande wake, Inter Miami anayocheza Lionel Messi imempa nyota huyo mkataba wa miaka miwili utakaofikia ukomo Desemba, 2027.

Reguilon alisajiliwa na Tottenham mwaka 2020 akitokea Madrid lakini aliishia kutolewa kwa mkopo katika klabu za Manchester United, Atletico Madrid na Brentford.

Kwa miaka yake mitatu ya utumishi ndani ya Tottenham alicheza mechi 86 za Ligi Kuu na kufunga mabao mawili pekee.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba wake Inter Miami, Reguilon amesema: “Ndoto yangu ni kuendelea kushinda, kupata mataji yaliyokosekana.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img