12.6 C
New York

Glasner kocha mpya Chelsea?

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca, amekiri kuwa amepoteza ushawishi mbele ya mabosi wa klabu hiyo ya Magharibi mwa Jiji la London. Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton, Maresca alisema alikuwa kwenye wakati mgumu kwa saa 48, ikielezwa kuwa aliwekwa ‘kitimoto’ na uongozi wa Chelsea.

Ikumbukwe, kabla ya kuifunga Everton, Chelsea ilikuwa imecheza mechi nne bila kupata ushindi.
Kwa sasa, jina la Oliver Glasner ndilo linalotajwa zaidi, ambapo kocha huyo wa Crystal Palace anahusishwa na mikoba ya Maresca atafukuzwa Stamford Bridge.

Glasner raia wa Austria, atamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na tayari hana maelewano mazuri na mabosi wa Palace kutokana na ‘ubahili’ wao katika soko la usajili.

Hivyo, ni wazi kocha huyo aliyeipa Palace taji la FA, pia akiwa na rekodi ya kutwaa Ligi ya Europa akiionao Frankfurt, atakataa mkataba mpya. Wakati huo huo, Liam Rosenior ni kocha mwingine anayetajwa Stamford Bridge. Anainoa Strasbourg ya Ufaransa na aliwahi kufanya kazi England akiwa na Hull City.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img