12.6 C
New York

Amorim, Mainoo kukutana mezani

Published:

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim, amesema atakutana kwenye meza ya mazungumzo na kiungo wa timu hiyo, Kobbie Mainoo.

Amorim anataka kuzungumza na kinda huyo ili kujadili hatima yake wakati huu akihusishwa na mpango wa kuondoka kwa mkopo ifikapo Januari, mwakani.

Mainoo aliomba kuondoka kwa mkopo tangu mwishoni mwa msimu uliopita lakini Man United iligoma kumwachia raia huyo wa England.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, hajaanza kikosi cha kwanza cha Man United tangu msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL) uanze.

Amorim amekuwa akisisitiza kuwa Mainoo anapaswa kubaki Old Trafford na kupigania namba mbele ya nahodha wa kikosi, Bruno Fernandes.

Hata hivyo, kocha huyo amekuwa akilaamikiwa kwa kile wachambuzi wa EPL wanachodai kuwa anakiua kipaji cha ‘dogo’ huyo.

Napoli imeonesha nia ya kumsajili na inaripotiwa kusubiri hatima ya mazungumzo yake na Amorim yanayotarajiwa kufanyika wiki hii.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img