12.6 C
New York

Madrid yamtaka Dalot wa United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

REAL Madrid wameripotiwa kuanza kuihangaikia saini ya beki wa Manchester United, Diogo Dalot, na watajaribu kumsajili ifikapo mwakani.

Dalot ameshacheza mechi 224 akiwa na jezi za Man United, zikiwamo 14 alizoshuka dimbani msimu huu.
Nyota huyo amekuwa akitumika katika nafasi zote za beki wa pembeni. Amecheza kulia na kushoto mara 13 msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Kwa mujibu wa mtandao wa Team talk, Mkurugenzi wa Ufundi wa Man United, Jason Wilcox, amepanga kumpiga bei mwishoni mwa msimu huu.

Mkataba wake wa sasa Old Trafford utafikia ukomo mwaka 2028 na kipo kipengele kinachomruhusu kuongeza mwingine wa miezi 12.

Katika kile kinachowasukuma kumuuza, mabosi wa Man United wanahofia Dalot atataka kuongezwa mshahara ili kusaini mkataba mpya klabuni hapo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img