18.1 C
New York

UNICEF: Kipindupindu kimeua watoto 340 DRC

Published:

KINSHASA, DRC

SHIRIKA la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeeleza kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inapitia kipindi kigumu zaidi kuwahi kutokea kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.

Takwimu za UNICEF za kuanzia Januari, mwaka huu, zinaonesha kuwa tayari kuna wagonjwa 64,427 wa kipindupindu, huku vifo vikiwa ni 1,888.

Kati ya 1,888 waliopoteza maisha, 340 ni watoto, kwa mujibu wa ripoti mpya hiyo ya Shirika hilo.
Ifahamike kuwa majimbo 17 kati ya 26 ya DRC yameripoti kuathiriwa na ugonjwa huo wa mlipuko.

Katika ripoti yake, UNICEF imeeleza kuwa watoto 16 kati ya 62 waliopata ugonjwa huo wakiwa kwenye kituo cha kulea yatima mjini Kinshasa, wamefariki.

“Watoto wa Congo hawapaswi kuathiriwa kiasi hiki na ugonjwa unaoepukika,” amesema Msemaji wa UNICEF, John Agbor.

UNICEF imetenga Dola za Marekani milioni sita katika mipango yake ya mwakani ya kukabiliana na ugonjwa huo nchini DRC.

“Kama hakutokuwa na nguvu ya ziada ya bajeti na mikakati, maisha ya wengi yataendelea kupotea,” amesisitiza Agbor. Kwa upande wake, Serikali ya DRC imetenga bajeti ya Dola milioni 192 kukabiliana na kipindupindu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img