12.6 C
New York

Ramos atajwa Old Trafford

Published:

MANCHESTER, Uingereza

ZIMEIBUKA ripoti zinazoihusisha Manchester United na beki wa kati wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Sergio Ramos.

Ramos mwenye umri wa miaka 39, hana timu kwa sasa baada ya hivi karibuni kuachana na Monterrey ya Ligi Kuu nchini Mexico.

Taarifa zinaeleza kuwa kocha Ruben Amorim anahitaji beki mzoefu, ambaye atakuwa kiongozi kwenye safu yake ya ulinzi inayoyumba msimu huu.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa bado hakuna mazungumzo yaliyofanyika kati ya Man United na mlinzi huyo wa zamani wa Sevilla.

Wakati huo huo, zipo taarifa zinazodai kuwa uwezekano ni mdogo kwa mabingwa hao mara 20 wa taji la Ligi Kuu ya England (EPL) kumsajili Ramos hapo Januari, mwakani.

Kwa upande wake, Ramos ameweka wazi kuwa bado hajafikiria kustaafu, na badala yake anasubiri ofa itakayompa mwelekeo mpya katika safari yake ya maisha ya soka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img