12.6 C
New York

Martinez kuziba pengo la Lewandowski?

Published:

MILAN, Italia

MSHAMBULIAJI wa kati wa Inter Milan, Lautaro Martinez, ameonesha kuvutiwa na mpango wa kwenda kuziba pengo la Robert Lewandowski.

Barcelona wameripotiwa kuanza kusaka mbadala wa Lewandowski anayetarajiwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Martinez mwenye umri wa miaka 28, amekuwa na kiwango bora msimu huu, ambapo amefunga mabao 11 katika mechi 19, yakiwamo matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa ujumla, nyota huyo wa kimataifa wa Argentina ameingia kambani mara 164 na kutoa ‘asisti’ 52 katika michezo yake 354 akiwa na jezi za Inter Milan.

Kwa upande mwingine, amekuwa pia na mchango mkubwa akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina, akifunga mabao 36 katika mechi 75.

Mbali ya Martinez, Barcelona wamekuwa pia wakihusishwa na Harry Kane na Julian Alvarez katika mpango wao wa kuziba pengo la Lewandowski.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img