LONDON, Uingereza
UNAMKUMBUKA Bruno Lage? Aliwahi kufanya kazi Ligi Kuu ya England akiwa na Wolves lakini sasa hana kibarua tangu alipofukuzwa Benfica na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.
Akiwa ameshinda tatu na kupoteza moja tu ya Ligi Kuu ya Ureno, Lage alifukuzwa baada ya Benfica kufungwa na Qarabag katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Thiago Motta ni kocha mwingine asiye na kibarua kwa sasa. Ana umri wa miaka 42 na alifuzukwa na Juventus mapema mwaka huu na nafasi yake kupewa Igor Tudor.
Motta raia wa Italia, amekataa ofa ya kuzinoa timu za taifa za Serbia na Ugiriki. Pia, aligoma kupokea ofa ya Spartak Moscow ya Urusi.
Erik ten Hag aliyewahi kuinoa Manchester United naye hana kibarua tangu alipotimuliwa na Bayer Leverkusen akiwa amefanya kazi kwa siku 62 tu.
Wakati huo huo, Ole Gunnar Solskjaer naye yuko benchi kwa sasa. Alitimuliwa na Besiktas ya Uturuki baada ya timu hiyo kufungwa na Lausanne katika mchezo wa Europa Conference.
Ni kama ilivyo kwa Edin Terzic, ambaye aliiongoza Borussia Dortmund kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita. Kwa nyakati tofauti, Roma na Brentford zimekuwa zikihusishwa na huduma ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 42.
Makocha wengine ni Ange Postecoglou, Brendan Rodgers, Zinedine Zidane, Gareth Southgate na Xavi.


