12.7 C
New York

Alexander‑Arnold nje miezi miwili Madrid

Published:

MADRID, Hispania

BEKI wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Trent Alexander‑Arnold, atakuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili akiuguza majeraha ya paja.

Mlinzi wa kulia huyo aliumia katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) dhidi ya Athletic Bilbao.
Ukiwa ni mchezo wake wa 11 tu msimu huu wa La Liga kutokana na majeraha, Alexander‑Arnold alitoa ‘asisti’ katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao hao.

Alexander-Arnold alipata majeraha hayo katika dakika ya 10 ya kipindi cha pili, ambapo aliondoshwa uwanjani kwa msaada wa madaktari.

Kwa mujibu wa chanzo kilichozungumza na kituo cha runinga cha BBC Sport, nyota huyo wa zamani wa Liverpool atakuwa nje ya dimba kwa takribani wiki nane.

Aidha, hilo ni pigo jingine Madrid kwani Alexander-Arnold anaungana na Dani Carvajal na Federico Valverde, ambao nao ni majeruhi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img