12.7 C
New York

Onana atemwa kikosini Cameroon

Published:

YOUNDE, Cameroon

MLINDA mlango wa Manchester United anayecheza kwa mkopo Trabzonspor ya Uturuki, Andre Onana, hajaitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon. Cameroon imeita kikosi kwa ajili ya maandalizi ya fainali zijazo za Mataifa ya Afrika zitakazoanza kutimua vumbi Desemba 21, mwaka huu, na kufikia tamati Januari 18, mwakani.

Onana mwenye umri wa miaka 29, amecheza mechi tatu za Cameroon msimu huu, mbili zikimalizika kwa timu hiyo kufungwa. Mechi ya mwisho ni ile waliyofungwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwakani.

Huku jina la Onana likikosekana, makipa walioitwa kikosini ni Simon Omossola, Devis Epassy, Simon Ngapandouetnbu na Edouard Sombang. Katika hatua nyingine, kikosi hicho kimewajumuhisha mshambuliaji wa Manchester United, Bryan Mbeumo, na kiungo wa Brighton, Carlos Baleba.

Hivi karibuni, baada ya mkongwe Samuel Eto’o kushinda awamu yake ya pili ya kuliongoza Shirikisho la Soka la Cameroon, alimtimua kocha wa timu hiyo, Marc Brys.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img