12.7 C
New York

Hawa hapa sita watakaong’oka Liverpool

Published:

MERSEYSIDE, England

ZIMEKUWAPO taarifa za Arne Slot kuondoka Liverpool, ikielezwa kuwa huenda mabosi wa klabu hiyo watamfungashia virago. Taarifa za kocha huyo wa kimataifa wa Uholanzi kufutwa kazi ziliiongezeka kwa kasi baada ya Liverpool kufungwa mabao 4-1 na Ajax, kikiwa ni kichapo cha tatu mfululizo.

Ikaelezwa, uwezekano ni mkubwa kwa Slot kufukuzwa hata kabla ya kumaliza mkataba wake hapo mwakani.
Kwa upande mwingine, winga wa kimataifa wa Italia, Federico Chiesa, naye anahusishwa na mlango wa kutokea pale Anfield.

Chiesa alitarajiwa kuondoka Liverpool tangu wakati wa usajili wa kiangazi, mwaka huu, akihusishwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu ya Italia (Serie A). Joe Gomez, beki anayesifika kwa uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi uwanjani, naye huenda akaondoka. Anahusishwa zaidi na vigogo wa Serie A, AC Milan.

Gomez amekosa mechi nyingi za Liverpool, hiyo ikitokana na wimbi la majeraha. Taarifa za kuondoka kwake zinachangiwa na kitendo cha Liverpool kuiwinda saini ya nahodha wa Crystal Palace, Marc Guehi.

Ibrahima Konate naye yuko mbioni kuondoka Anfield, licha ya Real Madrid imeripotiwa kuachana na mpango wa kumsajili baada ya kiwango chake kibovu msimu huu. Wakati huo huo, zipo taarifa za beki wa kushoto, Andy Robertson. Naye ni miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kufungasha virago na kutimka Liverpool.

Alikaribia kujiunga na Atletico Madrid miezi michache iliyopita na sasa anapata wakati mgumu kuingia kikosini kutokana na ushindani wa namba kutoka kwa Milos Kerkez na Kostas Tsimikas. Mohamed Salah naye huenda akaondoka. Kwa siku za hivi karibuni, mshambuliaji huyo ameonekana kupoteza ubora wake ndani ya uwanja.
Kama ilivyokuwa wakati wa dirisha kubwa la usajili lililopita, klabu tajiri za Ligi Kuu ya Saudi Arabia zinaitolea macho saini ya ‘Mo’ Salah.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img