10.1 C
New York

Singapore yaongoza kwa usalama duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
UTAFITI wa hivi karibuni uliofanywa katika mataifa 144 duniani umeitaja Singapore kuwa ndiyo kinara linapokuja suala la usalama.
Singapore, Taifa la barani Asia, limeshika nafasi hiyo kutokana na kiwango kidogo cha matukio ya uhalifu, sambamba na uimara wa mamlaka zake katika kusimamia sheria.
Watafiti walichunguza namna raia wa kila nchi wanavyojisikia huru kutembea katika nchi zao nyakati za usiku. Utafiti ulihusisha mahojiano na watu zaidi ya 144,000.
Mbaya zaidi kwa Bara la Afrika, Taifa la Afrika Kusini imeshika nafasi ya mwisho katika orodha hiyo, kwa mujibu wa utafiti huo wa Taasisi ya Gallup.
Baada ya Singapore, ambayo asilimia 98 ya watu wake waliohojiwa walisema hawahofii kutembea nyakati za usiku, Tajikistan inashika nafasi ya pili kwa asilimia 95.
Mataifa mengine yenye kiwango kizuri cha usalama kwa raia wake ni China na Oman (94%), Saudi Arabia (93%), Kuwait na Norway (91%), na Umoja wa Falme za Kiarabu (90%).
Wakati huo huo, ukiacha Afrika Kusini, ambayo iko mkiani kwa asilimia 33, mataifa mengine yaliyo na kiwango kisichoridhisha cha usalama ni Lesotho na Botswana (34%).
Pia, yapo mataifa ya Liberia (37%), Ecuador (38%), Chile (39%), Zimbabwe na Eswatini (40%), na Myanmar na Chad (41%).
Kwa upande mwingine, licha ya machafuko ya kisiasa katika maeneo mengi, asilimia 73 ya watu waliohojiwa walikiri kuwa hawana wasiwasi kutembea nyakati za usiku katika nchi zao.
Kiwango hicho cha usalama duniani ni kikubwa zaidi, ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2006, ambapo ilikuwa ni asilimia 63.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img