9 C
New York

Wanne wafariki kanisa likichomwa moto

Published:

MICHIGAN, Marekani
MTU asiyefahamika amechoma moto kanisa na kusababisha vifo vya watu wanne waliokuwa ndani wakati wa ibada ya Jumapili ya wiki iliyopita.
Hata hivyo, Thomas Jacob Sanford, mwanaume mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Burton, ambaye ndiye muhusika wa tukio hilo, naye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Aidha, taarifa ya polisi inaeleza kuwa Jacob Sanford alifika nje ya Kanisa la Michigan na kuanza kumimina risasi, kabla ya jengo hilo kuwaka moto wakati mamia ya waumini wakiendelea na ibada.
Lakini, kwa upande wao, polisi wameeleza kuwa bado uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha Jacob Sanford kufanya tukio hilo.
Tukio hilo limevuta hisia za Rais Donald Trump, ambaye amesema huo ni mwendelezo wa mashambulizi dhidi ya waumini wa Dini ya Ukiristo nchini Marekani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img