Na Mwandishi Wetu
Mgombea wa udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata Kunduchi, Michael Urio leo Agosti 18, 2025 amechukua fomu ya kutetea nafasi yake katika ofisi ya Mtendaji wa kata hiyo jijini Dar es Salaam.
Urio ambaye alikuwa diwani wa kata hiyo na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, aliibuka kidedea katika kura za maoni, akiongoza kwa kura za maoni 257 kati kura 789 zilizopigwa, huku aliyemfuatia ni Joyce Haule 250, Emmanuel Mkuchu (240) Hashim Komba (30) Happiness Kinyaha (12).

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo, Urio aliwashukuru wananchi wa Kunduchi na CCM kwa kumuamini na kumpa ridhaa kwa mara nyingine ya kugombea katika uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025.
Amesema jukumu kubwa lililopo mbele yake ni kuhakikisha wanapata kura nyingi kwa mgombea Urais wa chama hicho, Dk. Samia Suluhu Hassani na mgombea mwenza Dk. Emmanuel Nchimbi pamoja na Mbunge atakayepitishwa na CCM.


