JAKARTA, Indonesia
WATU zaidi ya 360, wakiwamo wanafunzi, wameugua ghafla baada ya kupata chakula cha bure kinachotolewa shuleni mjini Sragen.
Chakula hicho ni sehemu ya programu ya Rais Prabowo Subianto, ambapo shule zimetakiwa kutoa chakula bila malipo.
Wizdan Ridho Abimanyu, ambaye ni mwanafunzi, anasema alianza kusumbuliwa na tumbo usiku, muda mfupi tu baada ya kumaliza kula.
Programu hiyo ya chakula cha bure shuleni imeshawafikia watu zaidi ya milioni 15, huku lengo likiwa ni milioni 83 kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Hata hivyo, tangu kuanzishwa kwa programu hiyo, yamekuwapo matukio mengi ya watu wanaokula kujikuta wakiumwa ghafla.
Published:


