DARFUR, Sudan
UGONJWA wa kipindupindu umesababisha vifo vya watu 40 ndani ya wiki moja nchini Sudan, huku vita vinavyoendelea vikihusishwa na tatizo hilo.
Vita inayoendelea kati ya Serikali na waasi wa Kundi la Rapid Support Forces (RSF) imesababisha uhaba wa maji, huduma za afya na misaada ya kinibadamu.
Kwa mujibu wa ripoti ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), vifo vitakanavyo na kipindupindu vimefikia 2,470 kufikia Agosti 11, mwaka huu.
Licha ya vifo, madaktari wa MSF wameeleza kuwa wameshahudumia wagonjwa wa kipindupindu zaidi ya 2,300 ndani ya wiki moja.
MSF, kwa upande mwingine, imeataja wanawake, watoto na wazee kuwa ndiyo wahanga wakubwa wa ugonjwa huo.
Watu zaidi ya 40,000 wameripotiwa kupoteza maisha, huku milioni 12 wakikimbia makazi kutokana na vita hiyo kati ya wanajeshi wa Serikali na wapiganaji wa RSF.
Published:


