12.5 C
New York

Ten Hag amzuia Xhaka kurudi England

Published:

MUNICH, Ujerumani
KOCHA wa Bayer Leverkusen, Erik ten Hag, ameweka wazi kuwa kiungo wake raia wa Uswis,Granit Xhaka, hauzwi.
Xhaka aliyewahi kukipiga Arsenal, anahusishwa na mpango wa kurejea England, safari hii akiwindwa na Sunderland.
Mwanzoni mwa wiki hii, wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alisema tayari wameshakubaliana baadhi ya mambo na klabu hiyo.
Hata hivyo, baada ya kuwapiga bei Florian Wirtz na Jeremie Frimpong waliotua Liverpool, achilia mbali Jonathan Tah aliyetimkia Bayern Munich, Leverkusen haiku tayari kumpoteza Xhaka.
Akizungumzia hilo, kocha Ten Hag alisema: “Wakala anaweza kusema chochote lakini tayari klabu imeshapoteza wachezaji muhimu watatu.
“Hatutoruhusu mchezaji mwingine yeyote kuondoka, haitowezekana. Iko wazi, kwamba Granit ni kiongozi na alisaini mkataba wa miaka mitano na sasa amebakiza mitatu. Ni mchezaji muhimu mno kwetu kumwacha aondoke.”
Nyota huyo aliitumikia Arsenal kwa miaka saba akiwa Ligi Kuu ya England, kabla ya kujiunga na Leverkusen mwaka 2023.
Katika msimu wake wa kwanza, Leverkusen ilitwaa taji la Bundesliga chini ya kocha Xabi Alonso, ambaye naye ameondoka na kujiunga na Real Madrid.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img