LONDON, England
CHELSEA wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Uholanzi, Xavi Simons.
Baada ya kumuuza Noni Madueke aliyejiunga na Arsenal kwa Pauni milioni 52, Chelsea wameongeza Pauni milioni 8 kuishawishi RB Leipzig imwachie staa huyo.
Taarifa ziko wazi na zinaeleza kuwa tayari Blues wameshamalizana na Simons juu ya masilahi binafsi na sasa kilichobaki mazungumzo yanayoendelea kati yao na RB Leipzig.
Katika kuishawishi zaidi, Chelsea wako tayari kuweka fedha, pamoja na Carney Chukwuemeka ili RB Leipzig ikubali kuwapa Simons mwenye umri wa miaka 22.
Simons alikuwa moto msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), ambapo alifunga mabao 10 na kutoa ‘asisti’ saba katika michezo 25.
Mbali ya Chelsea, pia wapinzani wao wa London, Arsenal, nao wanatajwa kuitolea macho saini ya mchezaji huyo wa zamani wa PSG.
Published:


