24.2 C
New York

Rodri awindwa Madrid, atengewa bil. 348/-

Published:

MADRID, Hispania
REAL Madrid wametenga Pauni milioni 100 (zaidi ya Sh bil. 348 za Tanzania) za kuibomoa Manchester City kwa kumchukua kiungo wao, Rodri.
Kocha mpya, Xabi Alonso, ndiye aliyewaambia mabosi wa Madrid kuwa anaihitaji huduma ya ‘mido’ huyo raia wa Hispania.
Hii inaweza kuwa Habari mbaya kwa kocha wa Man City, Pep Guardiola, ambaye Rodri ni miongoni wa wachezaji muhimu zaidi kwenye kikosi chake.
Msimu uliopita, Rodri (29), alikosekana kwa muda mrefu kutokana na majeraha na hiyo ilichangia kwa kiasi kikubwa Man City kulikosa taji la Ligi Kuu ya England.
Kwa upande wao, mabosi wa Madrid wanaamini itakuwa rahisi kwa Rodri kukubali kurudi nyumbani baada ya miaka sita kupita tangu alipoondoka Atletico Madrid.

Related articles

Recent articles