MANCHESTER, England
BAADA ya kutangazwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Barcelona, Marcus Rashford amesema anajisikia yuko nyumbani.
Rashford mwenye umri wa miaka 27, amejiunga na Barca kwa mkopo wa miezi 12 akitokea England alikokuwa akiitumikia Manchester United.
Kwa mujibu wa mkataba wake, Barca wataruhusiwa kumsajili moja kwa moja kwa kuipa Man United kiasi cha Pauni milioni 30.
“Nimefurahi sana,” alisema Rashford na kuongeza: “Ni klabu ambayo ndoto za watu hutimia, wanatwaa mataji.
“Najisikia niko nyumbani. Sababu nyingine iliyonifanya nije ni kwamba hii ni sehemu sahihi kwa wachezaji wakubwa kuonesha vipaji vyao.”
Nyota huyo anakuwa mchezaji wa kwanza raia wa England kusajiliwa na vigogo hao wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) tangu Gary Lineker aliyefanya hivyo mwaka 1986.
Mara ya mwisho kwa Rashford kuitumikia Man United ilikuwa Desemba, mwaka jana, na msimu uliopita aliumalizia Aston Villa kwa mkopo.
Published:


