12.5 C
New York

Maguire aachwa Man United ikielekea Marekani

Published:

MANCHESTER, England
BEKI wa kati, Harry Maguire, hajaongozana na kikosi cha Manchester United kilichoelekea Chicago, Marekani, kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao.
Maguire mwenye umri wa miaka 32, hakuwa sehemu ya wachezaji 32 waliosafiri leo, ikielezwa kuwa amekosekana kutokana na sababu za kifamilia.
Kwa mujibu wa ripoti, mlinzi huyo wa kimataifa wa England ataungana na wenzake Jumatano ya wiki hii.
Ikumbukwe, Maguire alitokea benchi katika mchezo wa kirafiki uliopita dhidi ya Leeds United lakini alitolewa baada ya dakika 30 tu, licha ya kutokuwa na majeraha.
Katika hatua nyingine, wachezaji wapya wa Man United, Bryan Mbeumo na Matheus Cunha, wameongozana na wenzao kwenda Marekani.
Hivi karibuni, Man United ‘itatesti mitambo’ kwa kuzivaa West Ham, Bournemouth na Everton.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img