MADRID, Hispania
KLABU ya Liverpool inafuatilia kwa karibu hatima ya staa wa Real Madrid, Rodrygo.
Kwa wiki za hivi karibuni, Rodrygo raia wa Brazil amekuwa akihusishwa na mlango wa kutokea Santiago Bernabeu.
Klabu kadhaa, ikiwamo Arsenal, nayo ipo kwenye orodha ya zile zinazojaribu kuinasa saini ya mchezaji huyo.
Kwa upande wa Liverpool, wao wanaamini staa huyo atawafaa endapo mshambuliaji wao, Luis Diaz, ataondoka.
Madrid wako tayari kumpiga bei Rodrygo, ingawa mshahara wake unaweza kuwa changamoto kwa klabu nyingi zinazomtaka.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, analipwa euro milioni 10 (zaidi ya Sh bil. 30 za Tanzania) kwa mwaka pale Madrid.
Published:


