LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Gabriel Magalhaes, anaamini msimu ujao ni wao katika kunyakua mataji.
Kwa miaka sita ya kocha Mikel Arteta, Arsenal wamebeba taji la FA pekee mwaka 2020.
Washika Bunduki wamemaliza katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa msimu wa tatu mfululizo.
Msimu uliopita, walikuwa na matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini safari yao ilikwamia hatua ya nusu fainali baada ya kuondoshwa na PSG.
Kwa upande mwingine, wangeweza kuwa mabingwa wa Kombe la Ligi (Carabao Cup) lakini walikwamia nusu fainali kwa kufungwa na Newcastle United.
Akizungumzia walivyojipanga msimu ujao, Gabriel alisema: “Akili yetu tumeielekeza katika kile anachokisema kocha. Nafikiri mwaka huu unaweza kuwa tofauti.”
Published:


